FUATILIA MWENENDO WA MAONGEZI
YA MKE WA WAZIRI NA TRAFIKI
YALIYOPELEKEA ASKARI HUYO
KUPANDISHWA CHEO.
Kauli na sentensi mbovu za matusi anazodaiwa
kutoa mke wa Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa, Dk. Augustine Mahiga kwa askari wa
kikosi cha usalama barabarani imegeuka neema
kwa askari huyo.
Rais Dk. John Magufuli amemuagiza Kamishina
wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Ernest Mangu
kumpandisha cheo askari huyo ikiwa ni tuzo ya
kutukanwa akiwa kazini.
Alitoa agizo hilo juzi wakati alipokuwa akifungua
kikao cha makamanda wa polisi wa mikoa,
ambapo alisema tayari ameshamuonya waziri
ambaye mke wake alimtukana askari huyo.
?Hakuna kiongozi au familia ya kiongozi iliyoko
juu ya sheria,? alisema Rais Magufuli.
Katika sakata hilo, mke wa Mahiga anadaiwa
kumtukana askari huyo ambaye alikuwa katika
kituo chake cha kazi akitekeleza majukumu yake.
Mapema jana asubuhi, kwenye mitandao ya
kijamii ilisambazwa sauti ya mahojiano baina ya
askari huyo, mkuu wake wa kazi pamoja na mke
wa Mahiga.
Katika sauti hiyo, alisikika askari huyo akilalamikia
kitendo cha mke wa Mahiga kumtusi pale
alipotaka kumwandikia faini dereva wake kwa
kosa la kukanyaga alama ya pundamilia.
MAHOJIANO YALIVYOKUWA
Askari: Haloo afande? Lango 115 nimemkamata
akiwa amevuka ?zebra cross? wakati namtaka
?assign? kwa kosa alilofanya akaanza kunitukana?
anasema yeye ni mke wa waziri? nikamwambia
hili ni kosa la dereva, nikamuuliza anatukana kwa
sababu gani.
?Nikamwambia gari siiruhusu naipeleka kituoni.
Wakati namuamuru dereva apeleke gari kituoni
alitaka kuondoka, nikamnyang?anya funguo,?
alisema.
Upande wa pili: Kwa hiyo alikutukanaje?
Askari: Amenitukana kuwa mimi ni mshenzi, sina
akili? Anasema yeye ni mke wa Waziri Mahiga.
Upande wa pili: Sasa Mahiga ni waziri yupo juu ya
sheria?
Askari: Sijui afande kama yupo juu ya sheria,
mimi nimeamua kuizuia gari kituoni taratibu
zingine ziendelee.
Upande wa pili: Ok, huyo mama yupo hapo?
Askari: Ndio.
Upande wa pili: Nipe niongee naye. (kinapita
kitambo kidogo) Habari yako.
Mke wa Mahiga: Salama? huyu baba ni hivi?
mimi naitwa mama Mahiga, sikumtukana wala
sikusema hayo maneno ?anayoni-cot? ameamkaje
mimi sielewi, kitu nilichomwambia kwamba huyu
kijana alikuwa anakwenda moja kwa moja, mimi
nilikuwa na visenti kidogo.
Kijana akachepuka na sehemu anayotakiwa
kuchepuka ni hapa Namanga, akatusimamisha na
kusema eti alisimama kwenye ?zebra cross?,
nikamwambia sawa hilo ni kosa la kuelimishwa,
lakini sasa anamuandikia kwa kosa kama hilo? ni
dogo, ?very minor? (dogo sana), si la kumwandikia
lakini kama unaandika, andika hiyo Sh 30,000
sijui wanalipia wapi. Akatuelekeza, nikasema
mngeheshimika zaidi kama mngeweza
ku-?negotiate? kosa ?sub scouting? na nimeona
mapolisi wengi wanakosea hapo, kitu kidogo
mnakikuza kinakuwa kikubwa.
Upande wa pili: Unasema hilo ni ?very minor?,
unafahamu adhabu yake?
Mke wa Mahiga: Hapana? Basi nimekosa.
Upande wa pili: Hilo ni kosa kubwa na kama
dereva akimgonga mtu na kufikishwa mahakamani
ni kifungo jela, hakuna hata faini. Huyo dereva
anajua maana yake na anapokaribia anatakiwa
a-?slow down?.
Mke wa Mahiga: Hakuna ubishi lakini, nilitaka
aelewe (askari) mimi nimeendesha nchi nyingi,
naelewa sheria na nikamwomba amfundishe huyu
dereva.
Upande wa pili: Tufikie mahali tusifuge uovu, huyo
dereva afundishwe kwani hakwenda darasani?
Suala hilo tunategemea mtu yeyote aliyepita chuo
ni ?mandatory?, awe anafahamu. Huko nje
ulikotembelea naamini unajua jinsi
wanavyoheshimu na hasa hawa madereva wetu
huwa wanaheshimu, sasa ile kuchekeana inaleta
mazoea.
Nilitegemea kwamba amekosea na anachoagizwa
na askari afuate, vinginevyo kama (askari)
angekuwa ameomba rushwa ingekuwa kosa
lingine.
Hivyo naagiza dereva aadhibiwe, hatuko kutazama
nani ni nani. (Askari) huyo dereva muandikie faini,
hakuna aliye juu ya sheria.
Askari: Sawa mkuu, lakini nilitaka nimfungulie
mashtaka mahakamani.
Upande wa pili: Hayo sasa ni yako, lakini
muandikie hiyo faini kwa mujibu wa sheria.

No comments:
Post a Comment