Makala imeandikwa na Wynjones Kinye
(Mhadhiri chuo kikuu cha SAUT)
Naappreciate sana juhudi za Diamond katika
kuunyanyua muziki wa Tanzania kwa kuibua
vipaji vipya kama Harmonize, Raymond na
watakaofuata kama wapo.
Ni dhahiri kuwa kwa hili la kusimamia vijana
wawili tu kiasi kikubwa cha fedha kimetumika
na kinaendelea kutumika hasa ukizingatia
kuwa Diamond tayari ni mtu sensitive kwenye
quality ya product, na tunajua kuwa quality ni
gharama kubwa siku hizi kama sio siku zote.
Diamond amethubutu kuwekeza, kibiashara
tunategemea return katika kila unachofanya
‘kibiashara’ hivyo ni muhimu sana kufikiria
vitu vingi vya kuifanikisha biashara ukiachana
na mtaji. Hata kama una mtaji mkubwa na
fedha za ziada kuuendeleza mradi bado
failure iko pale kama hutotazama vitu vingine
kwa kina.
Licha ya nguvu nyingi anayoweka Diamond
kwenye muziki wa vijana wake ‘publicity na
video nzuri’ bado mimi nina hofu ya
kufanikiwa kwake kuwafikisha vijana wake
hawa chini ya label yake. Nilivumilia kulisema
hili baada ya kumsikiliza Harmonize, ila sasa
nimeshindwa kukaa nalo baada ya kumsikia
Raymond.
Naadmit kuwa hawa vijana Raymond na
Harmonize wana vipaji vikubwa, wana sauti
nzuri sana na ni waandishi vizuri lakini
wanakosa kitu cha kuwafanya kuwa brand.
Yupo mwandishi mmoja anaitwa Angela
Cross alisema…
“Your brand is the foundation of your
relationship with your audience – so be
mindful of who your audience is (and no, it’s
not “everyone”), what they want, and how you
can connect with and serve them.”
Najua brand ni neno pana na kila mtu
anaweza kulitetea kivyake kutokana na
mapenzi na uelewa kwenye suala husika,
vyovyote iwavyo niseme Diamond, Raymond,
na Harmonize ni “MTU MMOJA.” Yaani ukitoa
sauti zao (ambazo pia sasa zinaelekea
kufanana) vingine vyote ninafanana zaidi.
Hapa nazungumzia uandishi wao, mawazo
yao katika nyimbo, mtindo wa nyimbo zao,
uandishi wao, na strategies za kibiashara
ambazo naweza sema ni zile zile ambazo
ameziexperience Diamond. Sasa kwanini
tusifikirie brand kama ‘MUHURI’ ambao
utakutambulisha kwa audience kama zilivyo
documents zenye huo muhuri maofisini?
Haya, dalili zinaonyesha kuwa Richard
Mavoko ataingia kwenye Label ya Wasafi.
Ikitokea basi ni kheri lakini ni wazi pia kuwa
kutaongeza ‘mlundiko’ wa mfanano katika
muziki kwani hata mtu asiyefuatilia sana
anafahamu kuwa Richard kwa matoleo kadhaa
amekuwa akifanana sana kiuimbaji na
Diamond, hata uachiaji wa nyimbo zao
ulikuwa ukifuatana. Mbona yanaweza
kuepukika haya? Tazama Harmonize
anavyojaribu kuwa na attitude ya kwako.
Najua Diamond uko karibu sana na vijana
wako, naamini wako huru kuzungumza nawe,
uhuru huu sasa naona usifike kwenye muziki
unaofanya, naona vitu viwili hapa na sina
uhakika kipi ni kipi, kwamba vijana ni
mashabiki wa muziki wako hivyo wanajikuta
wanafanya unachofanya ama wewe ni bosi wa
vijana na unawaambia nini cha kufanya ili
ikurahisishie wewe kuwafanikishia ndoto zao.
Sijawahi kumsikia Raymond kabla, nilipata
shauku kubwa kumsikia baada ya kujua kuwa
yuko chini ya Wasafi, lakini shauku kubwa
zaidi niliipata baada ya kusikia kuwa ni
mtumiaji wa guitar katika uimbaji. Nilipata
mawazo kadhaa ya picha juu ya huyu jamaa
atakavyokuwa anaimba, niliamini angekuwa
tofauti na Harmonize, niliamini angekuja na
nyimbo tofauti na tulizozizoea siku hizi na
niseme tu kuwa nilikuwa so disappointed.
Wimbi hili halipo kwa Wasafi tu,. naona balaa
hili kutokea kwa Mkubwa na Wanawe. Angalia
uimbaji wa Yamoto Band na wale wadogo
zao, balaa linaendelea baada ya kumsikia
mshindi wa BSS ‘Kayumba’ ambaye pia ni
zao la Fella na sasa yupo chini ya usimamizi
unaomhusisha Fella na washirika wake.
Kayumba naye kaja na muziki uleule
unaofanywa na wenzake wanaomzunguka.
Diamond!! Kama umeamua kusimamia
wasanii nakushauri kuwaza ‘utofauti’, utofauti
na upya ni must katika soko la muziki
duniani kote especially sasa hivi, ni dhambi
kubwa kibiashara kuwa ‘COMMON.’ Uimbaji
na uandishi vya wasanii wako hakikisha
vinatofautiana na vya kwako. Kama umemudu
kuajiri mwalimu wa ‘kizungu’ kwa ajili ya
crew yako basi hautoshindwa kuajiri
mtaalamu wa kuwatengeneza tofauti vijana
wako kwa kila kitu, hii kazi usiifanye wewe
tafadhali.
Kwanini usitushangaze kwa kuja na vijana
wenye muziki wa kitofauti na uufanyao wewe?
Kuna ugumu gani kututengenezea kichwa
kingine cha RnB kikatoa changamoto kwa
wakina Ben Pol na Jux?
Kwanini usiufikirie muziki wa Grace Matata na
Damian Soul pia? Vipi kuhusu muziki mzuri
uliofanywa na Mandojo na Domokaya na
kushindwa kuvuka mipaka? Huoni kuwa hivi
vinavyotokea vinafanya tuchoke muziki (kitu
ambacho ni makosa makubwa), hatupaswi
kuuchoka muziki, fanyeni tusiuchoke muziki.
Nia yako ni nzuri sana Diamond na uzuri ni
kuwa unaimudu kabisa nia hiyo (kitu
ambacho ni muhimu sana), lakini kwanini
sasa ugharamike isivyostahiki kwa kutumia
nguvu tele kisa tu hujaweka mawazo yako/
yenu nje ya vitu visivyohusisha fedha? Hofu
yangu iko hapo zaidi, matumizi makubwa ya
pesa isivyostahiki.
Usisahau kutembelea na kusubscribe YouTube account Sun zedon kwa video mpya

No comments:
Post a Comment