Friday, May 6, 2016

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni aliingia kwa kushtukiza hospitalini M/Nyamala kama Mgonjwa, alicho

‘Hapa Kazi Tu’ msemo unaoendelea ‘kutrend’ na kufanywa kwa vitendo kwa kasi zaidi kwa watendaji wanaounda Serikali ya awamu ya tano.
Juzi mkuu wa Wilaya Kijana anayeiongoza Wilaya ‘Changamfu’ ya Kinondoni, Mh Ally Salum Hapi, alifanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya M/Nyamala kwa staili ya aina yake akijifanya kama mgonjwa anayehitaji Matibabu.
Mkuu huyo wa Wilaya amezungumza kupitia kipindi cha ‘Sunrise’ cha Times Fm, na kusema kuwa alifanya hivyo ili kubaini  changamoto na malalamiko ya wananchi wanazopata katika kuhudumiwa hospitalini hapo.
Hapi amebainisha changamoto alizokutana nazo kuwa ni pamoja na ukosefu wa Mashuka kwa kiasi kikubwa, Neti, Magodoro na Matabibu kuwa wachache hasa nyakati za usiku.
“Nilisikitika sana ni aibu Hospitali ya M/nyamala kukosa Neti, mashuka ya kutosha, kuna vitanda vingine watu wanalalia magodoro matupu” Alisema.
Katika kupambana na hali hiyo, amemuagiza Mkurugenzi mtendaji wa Hospitali ya M/Nyamala kuhakikisha anafanya kadri inavyowezekana ili kuhakikisha anapata mashuka na Neti, huku akiwataka wadau wa maendeleo kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha wanasaidia upatikanaji wa Magodoro na Vitanda.

No comments:

Post a Comment