Tuesday, October 25, 2016

TUMEKUWA CHAWA WAO VYA KUTOSHA SASA TUNAKWENDA KUWEKA HADHARANI KILA KITU


STAA wa filamu za kitanzani Jimmy Mafufu ameonyesha  hisia zake  kutokupendezwa na aina ya mfumo wa usambazaji unaotumiwa kwani  umekuwa ukiwagawa pande mbili tofauti
Mafufu amabaye ni Mkurugenzi  mtendaji  wa  J mafufu The Strong Film ameonyesha hisia zake kwa kuandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa facebook
kwa mujibu  Mafufu Kupitia ukurasa wake aliandika
" nawaonea huruma sana waigizaji wa mikoani tasnia imejaa ubinafsi mkubwa wasambazaji nao ni tatizo lingine kubwa wameendelea kuwagawa waigizaji ili wawatawale hawataki sura mpya kabisa lakini cha ajabu ninaowaonea huruma nao hawana umoja wanachukiana wao kwa wao hawakubaliani hata chembe kila mmoja anajua kuliko mwingine ni maombi yangu mungu awape macho ya rohoni waigizaji wote wa mikoani ili mkipewa macho hayo muisaidie tasnia hii kukua zaidi msichokijua ni kwamba tasnia inawategemea sana lakini mkiacha upuuzi wa kuchukiana na kutokukubaliana”
kwa msisitizo mafufu aliongeza
"muda umefika wa kila muigizaji tanzania kuliishi jasho lake hatuwezi kunyamaza wala kuendelea kumsujudia mtu anayetugawa ili atutawale yeye anakuwa tajiri kupitia filamu zetu sisi tunazidi kuwa masikini na watumwa wake hapana sasa nimejitolea kumfunga paka kengere inatosha sasa ulivyovuna kwa wizi na dhuruma vitunze maana unakwenda kuicha tasnia hii mikononi mwa wenyewe wito wangu kwa waigizaji wote tanzania mkisikia la mgambo limelia msiulize wapi kila mtu afunge kibwebwe tayari kwa kumkabili adui wa tasnia hii ya filamu ambaye mimi namjua na nitawaonyesha kwa vitendo muda sio mrefu muigizaji hawezi kuwa masikini duniani kote unaweza kuishi kifalme kwa filamu yako moja tu kifo cha kanumba na sajuki kiwe funzo lazima familia zetu zije ziishi vizuri siku tukiondoka duniani sio wahindi ndio wawe matajiri kupitia kazi zetu harafu familia zetu ziwe omba omba no no no sasa nakinukisha na nilishatoa angalizo mapema huwa sitaniii na sijasomea kushindwa mumeiibia sana serikali mumewaibia sana wasanii mumetugawa ili mututawale sasa inatosha nitatoka jasho la chuma ili waigizaji kila mahali tanzania waliishi jasho lao nimechaguliwa na kuaminiwa na waigizaji kuwa makamu mwenyekiti wa chama cha waigizaji tanzania na sasa nataka kuonyesha kwa nini nimekuwa kiongozi kwa vitendo anzeni kufungasha vilivyo vyenu kabla hamjaozea jela"
Mpaka  tunakufikishia habari hii Mafufu ameandika  ujumbe mwingine leo alfajiri akisema
"mapinduzi makubwa katika tasnia ya filamu yanakuja kila mwanafani mahali popote alipo tanzania atanufaika kupitia kipaji chake huyu mnyonyaji muda wake wa kufungasha virago vyake umetarajadi waigizaji anzeni kujiimarisha kisanaa na kuongeza weredi ili kuboresha kazi za sanaa naelewa tumewapoteza waigizaji wengi wazuri na wenye vipaji vya hali ya juu kutokana na ukilitimba wa wasambazaji uchwara tumegawanywa vya kutosha sasa kimenuka na soon la mgambo litapigwa kila muigizaji ajiandae tumechoka kumtumikia kafili.vipaji ni vyetu filamu ni zetu na tanzania ni yetu wametuchezea vya kutosha na tumekuwa chawa wao vya kutosha sasa tunakwenda kuweka hadharani kila kitu"

baadhi ya wadau wa filamu na waigizaji hasa walio chini walionyesha hisia zao kwa kutoa yao ya moyoni
Haidari Saidi Chumambili Mungu akusimamie Mwalimu Wangu maafufu umekuwa so tu mwanaharakati Bali mwenye kupigania mabadiriko ya kweli. Mungu awe nawe
Nai Nicholaus Go ahead na mungu atasimamia hilo...
Lunyiliko Kiyaulilo hatutakuwa nyuma yako kwa mapambano, bali tutakuwa bega kwa bega kiongozi wetu. na mungu atatusimamia maana anaona jitihada zinazofanyika. mungu yuko nasi

www.didasentertainment bado inaendelea na harakati za kumtafuta staa huyo kwa habari zaidi tutakufahamisha endelea kuwa nasi karibu

Monday, July 18, 2016

BIFU ZITO..... ! NEY HANA CHAKUNIPA LABDA MAKALIO


       Hit maker wa nyimbo ya Supu Gigy Money aka gigi mipesa ameibua mshike mshike kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuamua kumtolea uvivu msanii mwenzake mwenye sifa ya michano kwa wasanii wenzake hasa jinsi ya uwandishi wa ngoma zake kulenga sana michambo Ney Wamitego Ambaye hivi karibuni amefungiwa ngoma yake na balaza la sanaa BASATA inayo itwa " Pale kati"
Gigy ametokwa na povu zito  msikilize Gigy akifungukaaa...




 

Saturday, May 28, 2016

WEMA AANDIKA UJUMBE MFUPI KUJIBU SHIT YA HARMONIZE

 WEMA AMJIBU HARMONIZE BAADA YA KUMBA SHIT..

Mara baada ya video ambayo inasambaa mitandaoni ikimuonyesha Harmonaize akiimba huku akimtusi Wema Sepetu, Wema aamua kutoa ya moyoni kupitia mtandao wake wa kijamii wa Snapchart na kusema hivi   " UKIMYA WANGU NDO IMEKUWA FIMBO KWENU........KILA SIKU KUNISEMA TU........OH GOD PLEASE HELP ME......GIVE ME COURAGE TO OVERCOME THIS NEGATIVITY ........TATIZO KOSA LANGU SILIJUI NDO MAANA NAUMIA ......KOSA LANGU NI NINI HASWA......" alifungua mwanadada huyo.

Wednesday, May 18, 2016

MTITU AKUMBUKA ENZI NA MAMA MKUBWA NDANI YA ITV!

MUONGOZAJI wa filamu na mkurugenzi wa 5 Effect William Mtitu ‘Mtitu’ amerudisha mpira kwa kipa baada ya kurudi katika tamthilia na kuipa nguvu zaidi tofauti na filamu, Mtitu anasema misingi imara inapatikana kwa wasanii waliopitia katika tamthilia na kuingia katika filamu.

“Nilikuwa nikifanya utafiti nakugundua kuwa tamthilia imetoa vipaji vingi sana, nami nimeona bora nijikite huko na tumefanikiwa kuja na tamthilia kubwa sana ya Mama Kubwa, itakayoteka nyoyo za wapenzi wa maigizo,”
Mtitu anasema kuwa tamthilia hiyo itarushwa katika kituo cha ITV kila siku ya jumapili imewashirikisha wasanii kama Zebwe Mrisho, Alex Wasponga ‘Baba James’, Mariam Ismail, Getrude Mwita, na wasanii wengi wanaotamba katika tasnia ya filamu Swahilihood na imeongozwa na Mtitu .

KIMENUKA TENA MTANDAONI SHILOLE NA VANNESA MDEE MATUSI NJE NJE

Wanamziki wenye kiki hapa mjini Vanessa Mdee na Shishi bby Shilole wanarushiana matusi huko mitandaoni
story za chichini inasemekana inaweza kuwa ni mbinu za kuuzima wimbo wa alikiba ambao unatarajiwa kutoka tarehe 19 mwezi The rock Television. yaani kesho
ikumbukwe king kiba aliachia nyimbo miezi iliyopita aliyoshilikishwa na aliekuwa mpenzi  Shilole "Nuh Mziwanda" nyimbo ambayo maudhui na mashairi ya wiimbo huyo yalikua yakimlenga shilole.

Sunday, May 15, 2016

Dj huyu anadai yeye ndio baba wa dada yake Diamond, Esma Khan.


Dj huyu anadai yeye ndio baba wa dada yake Diamond, Esma Khan.

Kumekuwepo na usiri juu ya baba wa mdogo wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Esma Platnumz lakini huenda utata ukafika mwisho baada ya aliyekuwa DJ maarufu jijini Dar kuibuka na kudai kuwa ndiye aliyemzaa mtoto huyo na mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ akimpinga na kuamua kumuweka wazi baba halali wa Esma.

ILIKUWAJE?

Mapema wiki hii, mtu mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Jerry Kato mkazi wa Boko jijini Dar, alipiga simu kwenye chumba cha habari cha gazeti hili na kueleza kuwa, ana jambo linaloutesa moyo wake na kwamba amekuwa akitafuta kuwasiliana na Magazeti ya Global kwa muda mrefu hivyo angependa kukutana na mwandishi wetu ili atoe lililoukamata moyo wake.
WAKATUNA BOKO
Baada ya kufanyika mawasiliano, mwandishi wetu na Jerry walikutana na jamaa huyo huko Boko, nje kidogo ya Jiji la Dar ambapo alifunguka kuwa, yeye ndiye baba mzazi wa Esma Platnumz ila anashangaa mama wa mtoto huyo amekuwa akikwepa kumtambulisha.
MSIKIE MWENYEWE!
“Mimi naitwa Jerry Kato, nakumbuka mwaka 1982, nilikutana na huyu Sanura (Mama Diamond) pale Mbowe Hotel (sasa Bilicanas iliyopo Posta jijini Dar). Alikuja na jamaa mmoja anaitwa Spencer wakati mimi nafanya kazi ya U-DJ pale, tukatokea kupendana na kuanzisha uhusiano.
“Baada ya muda mrefu, Sanura alinasa ujauzito wakati huo mimi nakaa palepale Mbowe Hoteli, yeye anakaa Saigon (Kariakoo, Dar). Basi akawa anakuja pale hotelini na kunisumbua, si unajua tena mambo ya mimba.
….“Akaniambia alikuwa ananitafuta lakini aliambiwa nimekufa. Basi tukapanga tuonane, akaniambia niende mpaka Sinza (Mori) pale Big Bon, nikifika pale nimpigie simu atanifuata.
…..“Mara akaanza mazungumzo na kuniambia, ‘Jerry unakumbuka?’ nikamwambia nakumbuka, basi akaniambia, ‘sasa leo nataka nikuoneshe mtoto wako’. Akaita Esmaaa…, yule binti akaitika, akaja, akaita tena Nasibuuu, ndiyo akatokea Diamond…”.
“Hapo ndiyo akafanya utambulisho kwa Esma na kumwambia mimi ndiye baba yake hivyo asimsumbue tena. Na kweli nilipomtazama (Esma) anafanana na mama yangu mzazi hata rangi. Ikawa ni furaha tukakumbatiana na maisha yakaendelea.
Chanzo :Global Publishers

Saturday, May 14, 2016

PICHA:ZA MATUKIO MBALIMBALI KWENYE MSIBA WA KINYAMBE HUKO MBEYA




May 12 2016 taarifa za kifo cha msanii wa filamu za Comedy James Petro Nsemwaambaye wengi tunamfahamu kwa jina la ‘Kinyambe’  zilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii, kwa baadhi ya watu maarufu na wasanii kupost picha na kuonesha kuguswa na taarifa za kifo chake.

Ripota wa millardayo.com alifanikiwa kufika Uyole Mbeya na kukutana na baba mzazi wa marehemu mzee Petro Lugendelo Nsemwa na kutueleza nini kimepelekea kifo chaKinyambe ” Marehemu alikuwa anaumwa kwa kipindi cha miezi nane, alikuwa anasumbuliwa na pafu la upande mmoja lilikuwa alipumui vizuri”


Baba mzazi wa kinyambe
Kingine ambacho hufahamu ni kuwa ndani ya mwezi mmoja yaani siku kadhaa kabla yaKinyambe kufariki alimpoteza mtoto wake wa mwisho Bray James Petro aliyekuwa na umri wa miaka minne, ila jana May 11 2016 ndio alifariki baba mtu yaani Kinyambe. Jina halisi analotambulika katika familia yake ni James Petro Nsemwa na sio Mohammed Abdallah kama ambavyo wengi wanafahamu.