STAA wa filamu za kitanzani Jimmy Mafufu
ameonyesha hisia zake kutokupendezwa na aina ya mfumo wa usambazaji
unaotumiwa kwani umekuwa ukiwagawa pande
mbili tofauti
Mafufu amabaye ni Mkurugenzi mtendaji wa J mafufu The Strong Film
ameonyesha hisia zake kwa kuandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa facebook
kwa mujibu Mafufu Kupitia ukurasa wake aliandika
" nawaonea huruma sana waigizaji
wa mikoani tasnia imejaa ubinafsi mkubwa wasambazaji nao ni tatizo lingine
kubwa wameendelea kuwagawa waigizaji ili wawatawale hawataki sura mpya kabisa
lakini cha ajabu ninaowaonea huruma nao hawana umoja wanachukiana wao kwa wao
hawakubaliani hata chembe kila mmoja anajua kuliko mwingine ni maombi yangu
mungu awape macho ya rohoni waigizaji wote wa mikoani ili mkipewa macho hayo
muisaidie tasnia hii kukua zaidi msichokijua ni kwamba tasnia inawategemea sana
lakini mkiacha upuuzi wa kuchukiana na kutokukubaliana”
kwa msisitizo mafufu aliongeza
"muda umefika wa kila muigizaji
tanzania kuliishi jasho lake hatuwezi kunyamaza wala kuendelea kumsujudia mtu
anayetugawa ili atutawale yeye anakuwa tajiri kupitia filamu zetu sisi tunazidi
kuwa masikini na watumwa wake hapana sasa nimejitolea kumfunga paka kengere
inatosha sasa ulivyovuna kwa wizi na dhuruma vitunze maana unakwenda kuicha
tasnia hii mikononi mwa wenyewe wito wangu kwa waigizaji wote tanzania mkisikia
la mgambo limelia msiulize wapi kila mtu afunge kibwebwe tayari kwa kumkabili adui wa tasnia hii ya filamu ambaye
mimi namjua na nitawaonyesha kwa vitendo muda sio mrefu muigizaji hawezi kuwa
masikini duniani kote unaweza kuishi kifalme kwa filamu yako moja tu kifo cha
kanumba na sajuki kiwe funzo lazima familia zetu zije ziishi vizuri siku
tukiondoka duniani sio wahindi ndio wawe matajiri kupitia kazi zetu harafu
familia zetu ziwe omba omba no no no sasa nakinukisha na nilishatoa angalizo
mapema huwa sitaniii na sijasomea kushindwa mumeiibia sana serikali mumewaibia
sana wasanii mumetugawa ili mututawale sasa inatosha nitatoka jasho la chuma
ili waigizaji kila mahali tanzania waliishi jasho lao nimechaguliwa na
kuaminiwa na waigizaji kuwa makamu mwenyekiti wa chama cha waigizaji tanzania
na sasa nataka kuonyesha kwa nini nimekuwa kiongozi kwa vitendo anzeni
kufungasha vilivyo vyenu kabla hamjaozea jela"
Mpaka tunakufikishia habari hii Mafufu ameandika ujumbe mwingine leo alfajiri akisema
"mapinduzi makubwa katika tasnia
ya filamu yanakuja kila mwanafani mahali popote alipo tanzania atanufaika
kupitia kipaji chake huyu mnyonyaji muda wake wa kufungasha virago vyake
umetarajadi waigizaji anzeni kujiimarisha kisanaa na kuongeza weredi ili
kuboresha kazi za sanaa naelewa tumewapoteza waigizaji wengi wazuri na wenye
vipaji vya hali ya juu kutokana na ukilitimba wa wasambazaji uchwara
tumegawanywa vya kutosha sasa kimenuka na soon la mgambo litapigwa kila muigizaji
ajiandae tumechoka kumtumikia kafili.vipaji ni vyetu filamu ni zetu na tanzania
ni yetu wametuchezea vya kutosha na tumekuwa chawa wao vya kutosha sasa
tunakwenda kuweka hadharani kila kitu"
baadhi ya wadau wa filamu na waigizaji
hasa walio chini walionyesha hisia zao kwa kutoa yao ya moyoni
Haidari Saidi Chumambili Mungu akusimamie Mwalimu Wangu
maafufu umekuwa so tu mwanaharakati Bali mwenye kupigania mabadiriko ya kweli.
Mungu awe nawe
Nai Nicholaus Go ahead na mungu atasimamia hilo...
Lunyiliko Kiyaulilo hatutakuwa nyuma yako kwa mapambano,
bali tutakuwa bega kwa bega kiongozi wetu. na mungu atatusimamia maana anaona
jitihada zinazofanyika. mungu yuko nasi
www.didasentertainment
bado inaendelea na harakati za kumtafuta staa huyo kwa habari zaidi tutakufahamisha
endelea kuwa nasi karibu

No comments:
Post a Comment