BONGO MUVI IMEKUFA AU NI MANENO YA MTAANI TU?
Juzi nimeshituka
sana baada ya rafiki yangu mmoja kuniambia kuwa kama kuna super star
ambaye anauwezo wa ku produce filamu na yupo ana shoot filamu kwa sasa
ni mtajie jina kama wapo hawazidi wawili! Nilishituka nikajiuliza kwa
nini? Nikapata shida sasa huenda Bongo muvi imekufa! Nikaanza kufanya
uchunguzi nikakuta kila producer ana shoot tamthilia. Haa nilishangaa
mastar waliotoka kwenye tamthilia wakiita ni maigizo wakaenda kushoot filamu ambazo pia hazikuwa na tofauti na maigizo wakirudi kufanya maigizo. Duuuh! Nikaanza kujiuliza maswali bila majibu.
Hivi wadau ni wapi tumekosea? Ni msanii, mzalishaji, msambazaji au
mnunuzi wa mwisho kachoka? Taratibu kumbukumbu zangu zikanirudisha miaka
minne iliyopita kabla Steven Kanumba hajafa ambapo struggle za
wasambazaji kumiliki wasanii ma star zilivyo pamba moto na mastar kutoa
vikwazo kwa waandaaji wadogo. Maana ulikuwa ukienda kutaka kufanya kazi
utajibiwa na mkataba steps mwingine na mkataba pilipili basi tu ilikuwa
vituko na wasio na mikataba pia walisema na wao wanamikataba mhuuu!
Nikakumbuka kipindi kizuri cha ushindani. Kipindia ambapo tulikuwa na
wasambazaji wa kutosha. Tulikuwa na Steps na Kapico pia kulikuwa na Pili
pili, Vishal na Famous Video, Ajay, Bajomba, Game 1st Quality, Churu
Peace, Mwananchi, Al- Liyamy, SAS"O" Splash, Gibs Video, Tolly wood,
Papazi, Proin, Whatever, GMC Wasanii,Beck Net, Criss Creation n.k hizi
zote zilikuwa na ushindani na kila kampuni ilitoa muvi moja kwa wiki.
Kampuni hizi zilikuwa ni kubwa na zilileta changamoto na kulifanya game
liwe hot. Na kama inavyojulikana kwenye ushindani yule mwenye mtaji
mkubwa aliwashinda wenzake. Akatumia mbinu zake kuteketeza wenzake leo
hii ule ushindani haupo si hakuna wengine, utashindana na nani bidhaa
inatoka sehemu moja. Mtu anataka awe peke yake! Radha ikapungua kwa
watazamaji watu wakawa wanafanya kazi kuwahi foleni si hakuna kwingine
pa kuuza.
Sasa mawazo yangu yakanirudisha ni nani kaua soko?
Unapeleka muvi leo inatoka baada ya miaka miwili! Kumbe ungepeleka
kwenye kampuni nyingine na ungeuza mapema! Duuh zile siku za ushindani
zilikuwa nzuri ndio maana maneno midomoni yakawa mengi watu wakiisifia
na kila mtu akahamasika kuwa msanii kwa nafasi yake.
Ukitazama
kabla ya Kifo cha Steven Kanumba kulikuwa na kampuni nyingi sana za
usambazaji tena zenye uwezo mkubwa ila baada ya kifo chake kampuni moja
moja ikaanza kupoteza uwezo wa kusambaza na kuishia kufunga kampuni.
Wakabaki wasambazaji wachache ambao walijikongoja na mpaka sasa
msambazaji akitoa muvi tatu unatakiwa kumheshimu wengi huishia mbili tu
chali. Mungu atunusuru! Swali ukitengeneza muvi unauza wapi? Mbona
wasanii mastar wanakimbia kufanya muvi? Kuna tatizo gani? Au ndio upepo
wa kukurupuka umeenda kwenye tamthilia? Au ni kwa sababu TV stations
zimeongezeka? Midomoni mwa maproducer wengi ni ku produce tamthilia kitu
ambacho kinahitaji bajeti kubwa kuliko muvi!
MUNGU BARIKI TASNIA YETU.

No comments:
Post a Comment