Vilio
vilitawala jana wakati zaidi ya nyumba 400 za wakazi wa Mtaa wa
Mloganzila,Kibamba katika Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam,
zilipokuwa zikibomolewa.Ubomoaji huo ulianza saa 4:00 asubuhi baada ya
mmiliki wa eneo hilo la ekari 33, Henry Kashangaki kushinda kesi dhidi
ya watu 11 wanaodaiwa kuvamia eneo hilo na kuwauzia wananchi wengine
ambao walijenga nyumba bila kufahamu undani wa eneo hilo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya waaathirika wa ubomoaji
huo, walisema taarifa za kutakiwa kuondoka katika eneo hilo kabla ya
kuvunjiwa nyumba zao, walizipata Aprili 30 mwaka huu na hawakupewa muda
wa kutosha kuondoa mali zao.
Mkazi mmoja ambaye hakutaka jina lake
lijulikane, alilalamikia kuwa hawakutendewa haki kwa vile haikuwa
rahisi kwa muda huo mfupi wa siku moja kuweza kuokoa mali zao.

No comments:
Post a Comment