Saturday, May 28, 2016

WEMA AANDIKA UJUMBE MFUPI KUJIBU SHIT YA HARMONIZE

 WEMA AMJIBU HARMONIZE BAADA YA KUMBA SHIT..

Mara baada ya video ambayo inasambaa mitandaoni ikimuonyesha Harmonaize akiimba huku akimtusi Wema Sepetu, Wema aamua kutoa ya moyoni kupitia mtandao wake wa kijamii wa Snapchart na kusema hivi   " UKIMYA WANGU NDO IMEKUWA FIMBO KWENU........KILA SIKU KUNISEMA TU........OH GOD PLEASE HELP ME......GIVE ME COURAGE TO OVERCOME THIS NEGATIVITY ........TATIZO KOSA LANGU SILIJUI NDO MAANA NAUMIA ......KOSA LANGU NI NINI HASWA......" alifungua mwanadada huyo.

Wednesday, May 18, 2016

MTITU AKUMBUKA ENZI NA MAMA MKUBWA NDANI YA ITV!

MUONGOZAJI wa filamu na mkurugenzi wa 5 Effect William Mtitu ‘Mtitu’ amerudisha mpira kwa kipa baada ya kurudi katika tamthilia na kuipa nguvu zaidi tofauti na filamu, Mtitu anasema misingi imara inapatikana kwa wasanii waliopitia katika tamthilia na kuingia katika filamu.

“Nilikuwa nikifanya utafiti nakugundua kuwa tamthilia imetoa vipaji vingi sana, nami nimeona bora nijikite huko na tumefanikiwa kuja na tamthilia kubwa sana ya Mama Kubwa, itakayoteka nyoyo za wapenzi wa maigizo,”
Mtitu anasema kuwa tamthilia hiyo itarushwa katika kituo cha ITV kila siku ya jumapili imewashirikisha wasanii kama Zebwe Mrisho, Alex Wasponga ‘Baba James’, Mariam Ismail, Getrude Mwita, na wasanii wengi wanaotamba katika tasnia ya filamu Swahilihood na imeongozwa na Mtitu .

KIMENUKA TENA MTANDAONI SHILOLE NA VANNESA MDEE MATUSI NJE NJE

Wanamziki wenye kiki hapa mjini Vanessa Mdee na Shishi bby Shilole wanarushiana matusi huko mitandaoni
story za chichini inasemekana inaweza kuwa ni mbinu za kuuzima wimbo wa alikiba ambao unatarajiwa kutoka tarehe 19 mwezi The rock Television. yaani kesho
ikumbukwe king kiba aliachia nyimbo miezi iliyopita aliyoshilikishwa na aliekuwa mpenzi  Shilole "Nuh Mziwanda" nyimbo ambayo maudhui na mashairi ya wiimbo huyo yalikua yakimlenga shilole.

Sunday, May 15, 2016

Dj huyu anadai yeye ndio baba wa dada yake Diamond, Esma Khan.


Dj huyu anadai yeye ndio baba wa dada yake Diamond, Esma Khan.

Kumekuwepo na usiri juu ya baba wa mdogo wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Esma Platnumz lakini huenda utata ukafika mwisho baada ya aliyekuwa DJ maarufu jijini Dar kuibuka na kudai kuwa ndiye aliyemzaa mtoto huyo na mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ akimpinga na kuamua kumuweka wazi baba halali wa Esma.

ILIKUWAJE?

Mapema wiki hii, mtu mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Jerry Kato mkazi wa Boko jijini Dar, alipiga simu kwenye chumba cha habari cha gazeti hili na kueleza kuwa, ana jambo linaloutesa moyo wake na kwamba amekuwa akitafuta kuwasiliana na Magazeti ya Global kwa muda mrefu hivyo angependa kukutana na mwandishi wetu ili atoe lililoukamata moyo wake.
WAKATUNA BOKO
Baada ya kufanyika mawasiliano, mwandishi wetu na Jerry walikutana na jamaa huyo huko Boko, nje kidogo ya Jiji la Dar ambapo alifunguka kuwa, yeye ndiye baba mzazi wa Esma Platnumz ila anashangaa mama wa mtoto huyo amekuwa akikwepa kumtambulisha.
MSIKIE MWENYEWE!
“Mimi naitwa Jerry Kato, nakumbuka mwaka 1982, nilikutana na huyu Sanura (Mama Diamond) pale Mbowe Hotel (sasa Bilicanas iliyopo Posta jijini Dar). Alikuja na jamaa mmoja anaitwa Spencer wakati mimi nafanya kazi ya U-DJ pale, tukatokea kupendana na kuanzisha uhusiano.
“Baada ya muda mrefu, Sanura alinasa ujauzito wakati huo mimi nakaa palepale Mbowe Hoteli, yeye anakaa Saigon (Kariakoo, Dar). Basi akawa anakuja pale hotelini na kunisumbua, si unajua tena mambo ya mimba.
….“Akaniambia alikuwa ananitafuta lakini aliambiwa nimekufa. Basi tukapanga tuonane, akaniambia niende mpaka Sinza (Mori) pale Big Bon, nikifika pale nimpigie simu atanifuata.
…..“Mara akaanza mazungumzo na kuniambia, ‘Jerry unakumbuka?’ nikamwambia nakumbuka, basi akaniambia, ‘sasa leo nataka nikuoneshe mtoto wako’. Akaita Esmaaa…, yule binti akaitika, akaja, akaita tena Nasibuuu, ndiyo akatokea Diamond…”.
“Hapo ndiyo akafanya utambulisho kwa Esma na kumwambia mimi ndiye baba yake hivyo asimsumbue tena. Na kweli nilipomtazama (Esma) anafanana na mama yangu mzazi hata rangi. Ikawa ni furaha tukakumbatiana na maisha yakaendelea.
Chanzo :Global Publishers

Saturday, May 14, 2016

PICHA:ZA MATUKIO MBALIMBALI KWENYE MSIBA WA KINYAMBE HUKO MBEYA




May 12 2016 taarifa za kifo cha msanii wa filamu za Comedy James Petro Nsemwaambaye wengi tunamfahamu kwa jina la ‘Kinyambe’  zilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii, kwa baadhi ya watu maarufu na wasanii kupost picha na kuonesha kuguswa na taarifa za kifo chake.

Ripota wa millardayo.com alifanikiwa kufika Uyole Mbeya na kukutana na baba mzazi wa marehemu mzee Petro Lugendelo Nsemwa na kutueleza nini kimepelekea kifo chaKinyambe ” Marehemu alikuwa anaumwa kwa kipindi cha miezi nane, alikuwa anasumbuliwa na pafu la upande mmoja lilikuwa alipumui vizuri”


Baba mzazi wa kinyambe
Kingine ambacho hufahamu ni kuwa ndani ya mwezi mmoja yaani siku kadhaa kabla yaKinyambe kufariki alimpoteza mtoto wake wa mwisho Bray James Petro aliyekuwa na umri wa miaka minne, ila jana May 11 2016 ndio alifariki baba mtu yaani Kinyambe. Jina halisi analotambulika katika familia yake ni James Petro Nsemwa na sio Mohammed Abdallah kama ambavyo wengi wanafahamu.

Friday, May 13, 2016

WAFAHAMU VIGOGO WA TANZANIA WALIO FICHA FEDHA NJE.

Panama papers: Majina ya Watanzania waliohifadhi fedha nje ya nchi yatajwa Kwa wale waliokuwa wansubiri kupekuwa kwenye database ya Panama papers kuona kama kuna vijogoo wa Afrika hususani Tanzania wameficha fedha wanaweza kupekuwa sasa. Kila kitu kimewekwa online. Baadhi ya majina ni; Hasnain Ahmed Hassanali Tanzania, United Republic of Panama Papers Mohamedraza Ahmed Hassanali Tanzania, United Republic of Panama Papers Ahmedirfan Mohamedraza Hassanali Tanzania, United Republic of Panama Papers MR. KASBIAN NURIEL CHIRICH Tanzania, United Republic of Panama Papers Mr. Azizi ROSTAM Tanzania, United Republic of Panama Papers Nawshad Ahmed Hassanali Tanzania, United Republic of Panama Papers JORGE MARITINO Tanzania, United Republic of Panama Papers EDUARDO MARTINO Tanzania, United Republic of Panama Papers JORGE MARTINO Tanzania, United Republic of Panama Papers EDUARDO MARITINO Tanzania, United Republic of Panama Papers JACEK MONLNIK ROGOYSKI Tanzania, United Republic of Panama Papers BOULDER MINING LIMITED Tanzania, United Republic of Panama Papers MRS. SUKAINA MANJI Tanzania, United Republic of Panama Papers Talal Mohamed Abood Tanzania, United Republic of Panama Papers Abbas Mohammed Jessa Tanzania, United Republic of Panama Papers NARENDRA VAGHJIBHAI PATEL Tanzania, United Republic of Panama Papers Ms. Zuzana Kovacicova Tanzania, United Republic of Panama Papers Mr. Eric PASANISI Tanzania, United Republic of Panama Papers SAJJAD MOHAMEDHUSSEIN VIRANI Tanzania, United Republic of Panama Papers Mr. Eric PASANISI Tanzania, United Republic of Panama Papers Mr. Suril Shah Tanzania, United Republic of Panama Papers Suril V. Shah Tanzania, United Republic of Panama Papers Mr Kalpesh Menhta Tanzania, United Republic of Panama Papers Roberta Thomaz de Mattos Brisolla Tanzania, United Republic of Panama Papers NICHOLAS CHARLES WILSON Tanzania, United Republic of Panama Papers SEYDOU KANE Tanzania, United Republic of Panama Papers KONSEL JAMES WAMBURA Tanzania, United Republic of Panama Papers Abbas Mohamed Jessa Tanzania, United Republic of Panama Papers SUN MINING LIMITED Tanzania, United Republic of Panama Papers Abdulaziz Mohamed Abood Tanzania, United Republic of Panama Papers ABBAS MOHAMMED JESSA Tanzania, United Republic of Panama Papers Mohamed Panju Jessa Tanzania, United Republic of Panama Papers Abbas Mohamed Jessa Tanzania, United Republic of Panama Papers HARIDATT VAGHJIBHAI PATEL Tanzania, United Republic of Panama Papers Fauzi Mohamed Abood Tanzania, United Republic of Panama Papers B.A. KOTECHA Tanzania, United Republic of Panama Papers R.D. KOTECHA Tanzania, United Republic of Panama Papers MRS. SUKAINA MANJI Tanzania, United Republic of Panama Papers SUKAINA MANJI AND YUSUF MANJI AS TRUSTEES OF THE MANJI FAMILY TRUST Tanzania, United Republic of Panama Papers ANIL VAGHJIBHAI PATEL Tanzania, United Republic of Panama Papers Mrs Kantaben Manibhai Chhotabhai Patel Tanzania, United Republic of Panama Papers MRS. ROSMINA KANANI Tanzania, United Republic of Panama Papers MR. DANIEL LITTMAN Tanzania, United Republic of Panama Papers Mrs. Aarti Puri Tanzania, United Republic of Panama Papers Mr. Eric PASANISI Tanzania, United Republic of Panama Papers Mr. Azizi ROSTAM Tanzania, United Republic of Panama Papers Andre Schmid Tanzania, United Republic of Offshore Leaks KANIZ MEHBUB MANJI Tanzania, United Republic of Offshore Leaks Mr. Stuart Hugh MacDonald Tanzania, United Republic of Offshore Leaks Mr Rameshchandra Chotalal Somani Tanzania, United Republic of Offshore Leaks Rameshchandra C. Somani Tanzania, United Republic of Offshore Leaks Mr. Rameshchandra C. Somani Tanzania, United Republic of Offshore Leaks MEHBUB YUSUFALI MANJI Tanzania, United Republic of Offshore Leaks Wengine ni; LIERVAAG, M. Tanzania, United Republic ofPanama Papers NICITERETSE, ROGER Tanzania, United Republic ofPanama Papers JAMES BABAN Tanzania, United Republic of, MauritiusPanama Papers WHEELOCK HOLDINGS LTD. 26-NOV-1996 British Virgin Islands Tanzania, United Republic of Panama Papers RICHMOND FINANCE CORPORATION 11-MAR-1986 Panama Tanzania, United Republic of Panama Papers EXPRO ENERGY LTD. 23-JUL-2014 British Virgin Islands Tanzania, United Republic of Panama Papers Vilevile zimepatikana anwani za watu 38 kati ya hao ambazo ni; 42 KWALE RD; OYSTER BAY; DAR ES SALAAM; TANZANIATanzania, United Republic ofPanama Papers 5060 Morogoro Road; Daresalam; TanzaniaTanzania, United Republic ofPanama Papers Av. De Mayo 701 piso 19; Buenos Aires; Argentine RepublicTanzania, United Republic ofPanama Papers C/O PLOT 40 KURASINI; TEMEKE DISTRICT; PO BOX 359; DAR ES SALAAM; TANZANLA Tanzania, United Republic ofPanama Papers DoB 18/10/1969 Slvak RepublicTanzania, United Republic ofPanama Papers FLAT NO. 5 1st FLOOR TANGANYIKA FLATS INDIRA GHANDI HOUSE PO BOX 1912 DARESSALAAM TANZANIA Tanzania, United Republic ofPanama Papers Kunduchi; Plot 52/53 - 21880 - DAR ES SALAAM; TanzaniaTanzania, United Republic ofPanama Papers Kunduchi; Plot 52/53 - 21

Friday, May 6, 2016

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni aliingia kwa kushtukiza hospitalini M/Nyamala kama Mgonjwa, alicho

‘Hapa Kazi Tu’ msemo unaoendelea ‘kutrend’ na kufanywa kwa vitendo kwa kasi zaidi kwa watendaji wanaounda Serikali ya awamu ya tano.
Juzi mkuu wa Wilaya Kijana anayeiongoza Wilaya ‘Changamfu’ ya Kinondoni, Mh Ally Salum Hapi, alifanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya M/Nyamala kwa staili ya aina yake akijifanya kama mgonjwa anayehitaji Matibabu.
Mkuu huyo wa Wilaya amezungumza kupitia kipindi cha ‘Sunrise’ cha Times Fm, na kusema kuwa alifanya hivyo ili kubaini  changamoto na malalamiko ya wananchi wanazopata katika kuhudumiwa hospitalini hapo.
Hapi amebainisha changamoto alizokutana nazo kuwa ni pamoja na ukosefu wa Mashuka kwa kiasi kikubwa, Neti, Magodoro na Matabibu kuwa wachache hasa nyakati za usiku.
“Nilisikitika sana ni aibu Hospitali ya M/nyamala kukosa Neti, mashuka ya kutosha, kuna vitanda vingine watu wanalalia magodoro matupu” Alisema.
Katika kupambana na hali hiyo, amemuagiza Mkurugenzi mtendaji wa Hospitali ya M/Nyamala kuhakikisha anafanya kadri inavyowezekana ili kuhakikisha anapata mashuka na Neti, huku akiwataka wadau wa maendeleo kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha wanasaidia upatikanaji wa Magodoro na Vitanda.

Wednesday, May 4, 2016

Waandishi wa habari nchini wametakiwa kufanya kazi zao kwa utaratibu na kufuata miiko na maadili ya taaluma yao na kutakiwa kutojiingiza katika mambo ambayo ni kinyume na taaluma ya uandishi wa habari.Hayo yalisemwa jana na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, yaliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Siasa (TAPOREA) na kufanyika jijini Dar es Salaam jana.
“Tasnia ya habari ina utaratibu wake na miiko yake na ninyi lazima mtii miiko hiyo…msijiingize katika mambo ambayo ni kinyume kabisa cha taaluma yenu,” alisema Sumaye. Sumaye alisema uhuru wa habari una pande mbili, hivyo mmoja usizuiwe kutafuta, kupokea na kusambaza habari na upande wa pili ni mwandishi kufanya kazi kwa kufuata utaalamu na miiko ya taaluma yenyewe.
Alisema mwandishi ukiandika habari za uongo bila kuzithibitisha ni makosa, lakini pia ni makosa kuandika kwa kumuandama mtu au kikundi kwa kumchafua kwa makusudi. Alisema mwandishi ukimwandika mtu vibaya kwa sababu umelipwa fedha; au ukiacha kuandika ukweli kwa sababu hiyo hiyo ya kulipwa fedha au ya kutishiwa, nayo ni makosa.

Tuesday, May 3, 2016

FUATILIA MWENENDO WA MAONGEZI
YA MKE WA WAZIRI NA TRAFIKI
YALIYOPELEKEA ASKARI HUYO
KUPANDISHWA CHEO.
Kauli na sentensi mbovu za matusi anazodaiwa
kutoa mke wa Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa, Dk. Augustine Mahiga kwa askari wa
kikosi cha usalama barabarani imegeuka neema
kwa askari huyo.
Rais Dk. John Magufuli amemuagiza Kamishina
wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Ernest Mangu
kumpandisha cheo askari huyo ikiwa ni tuzo ya
kutukanwa akiwa kazini.
Alitoa agizo hilo juzi wakati alipokuwa akifungua
kikao cha makamanda wa polisi wa mikoa,
ambapo alisema tayari ameshamuonya waziri
ambaye mke wake alimtukana askari huyo.
?Hakuna kiongozi au familia ya kiongozi iliyoko
juu ya sheria,? alisema Rais Magufuli.
Katika sakata hilo, mke wa Mahiga anadaiwa
kumtukana askari huyo ambaye alikuwa katika
kituo chake cha kazi akitekeleza majukumu yake.
Mapema jana asubuhi, kwenye mitandao ya
kijamii ilisambazwa sauti ya mahojiano baina ya
askari huyo, mkuu wake wa kazi pamoja na mke
wa Mahiga.
Katika sauti hiyo, alisikika askari huyo akilalamikia
kitendo cha mke wa Mahiga kumtusi pale
alipotaka kumwandikia faini dereva wake kwa
kosa la kukanyaga alama ya pundamilia.
MAHOJIANO YALIVYOKUWA
Askari: Haloo afande? Lango 115 nimemkamata
akiwa amevuka ?zebra cross? wakati namtaka
?assign? kwa kosa alilofanya akaanza kunitukana?
anasema yeye ni mke wa waziri? nikamwambia
hili ni kosa la dereva, nikamuuliza anatukana kwa
sababu gani.
?Nikamwambia gari siiruhusu naipeleka kituoni.
Wakati namuamuru dereva apeleke gari kituoni
alitaka kuondoka, nikamnyang?anya funguo,?
alisema.
Upande wa pili: Kwa hiyo alikutukanaje?
Askari: Amenitukana kuwa mimi ni mshenzi, sina
akili? Anasema yeye ni mke wa Waziri Mahiga.
Upande wa pili: Sasa Mahiga ni waziri yupo juu ya
sheria?
Askari: Sijui afande kama yupo juu ya sheria,
mimi nimeamua kuizuia gari kituoni taratibu
zingine ziendelee.
Upande wa pili: Ok, huyo mama yupo hapo?
Askari: Ndio.
Upande wa pili: Nipe niongee naye. (kinapita
kitambo kidogo) Habari yako.
Mke wa Mahiga: Salama? huyu baba ni hivi?
mimi naitwa mama Mahiga, sikumtukana wala
sikusema hayo maneno ?anayoni-cot? ameamkaje
mimi sielewi, kitu nilichomwambia kwamba huyu
kijana alikuwa anakwenda moja kwa moja, mimi
nilikuwa na visenti kidogo.
Kijana akachepuka na sehemu anayotakiwa
kuchepuka ni hapa Namanga, akatusimamisha na
kusema eti alisimama kwenye ?zebra cross?,
nikamwambia sawa hilo ni kosa la kuelimishwa,
lakini sasa anamuandikia kwa kosa kama hilo? ni
dogo, ?very minor? (dogo sana), si la kumwandikia
lakini kama unaandika, andika hiyo Sh 30,000
sijui wanalipia wapi. Akatuelekeza, nikasema
mngeheshimika zaidi kama mngeweza
ku-?negotiate? kosa ?sub scouting? na nimeona
mapolisi wengi wanakosea hapo, kitu kidogo
mnakikuza kinakuwa kikubwa.
Upande wa pili: Unasema hilo ni ?very minor?,
unafahamu adhabu yake?
Mke wa Mahiga: Hapana? Basi nimekosa.
Upande wa pili: Hilo ni kosa kubwa na kama
dereva akimgonga mtu na kufikishwa mahakamani
ni kifungo jela, hakuna hata faini. Huyo dereva
anajua maana yake na anapokaribia anatakiwa
a-?slow down?.
Mke wa Mahiga: Hakuna ubishi lakini, nilitaka
aelewe (askari) mimi nimeendesha nchi nyingi,
naelewa sheria na nikamwomba amfundishe huyu
dereva.
Upande wa pili: Tufikie mahali tusifuge uovu, huyo
dereva afundishwe kwani hakwenda darasani?
Suala hilo tunategemea mtu yeyote aliyepita chuo
ni ?mandatory?, awe anafahamu. Huko nje
ulikotembelea naamini unajua jinsi
wanavyoheshimu na hasa hawa madereva wetu
huwa wanaheshimu, sasa ile kuchekeana inaleta
mazoea.
Nilitegemea kwamba amekosea na anachoagizwa
na askari afuate, vinginevyo kama (askari)
angekuwa ameomba rushwa ingekuwa kosa
lingine.
Hivyo naagiza dereva aadhibiwe, hatuko kutazama
nani ni nani. (Askari) huyo dereva muandikie faini,
hakuna aliye juu ya sheria.
Askari: Sawa mkuu, lakini nilitaka nimfungulie
mashtaka mahakamani.
Upande wa pili: Hayo sasa ni yako, lakini
muandikie hiyo faini kwa mujibu wa sheria.
Vilio vilitawala jana wakati zaidi ya nyumba 400 za wakazi wa Mtaa wa Mloganzila,Kibamba katika Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam, zilipokuwa zikibomolewa.Ubomoaji huo ulianza saa 4:00 asubuhi baada ya mmiliki wa eneo hilo la ekari 33, Henry Kashangaki kushinda kesi dhidi ya watu 11 wanaodaiwa kuvamia eneo hilo na kuwauzia wananchi wengine ambao walijenga nyumba bila kufahamu undani wa eneo hilo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya waaathirika wa ubomoaji huo, walisema taarifa za kutakiwa kuondoka katika eneo hilo kabla ya kuvunjiwa nyumba zao, walizipata Aprili 30 mwaka huu na hawakupewa muda wa kutosha kuondoa mali zao.
Mkazi mmoja ambaye hakutaka jina lake lijulikane, alilalamikia kuwa hawakutendewa haki kwa vile haikuwa rahisi kwa muda huo mfupi wa siku moja kuweza kuokoa mali zao.

Sunday, May 1, 2016

MSIBA MWINGINE MKUBWA WAIKUMBA BONGO MOVIES

BONGO MUVI IMEKUFA AU NI MANENO YA MTAANI TU?
Juzi nimeshituka sana baada ya rafiki yangu mmoja kuniambia kuwa kama kuna super star ambaye anauwezo wa ku produce filamu na yupo ana shoot filamu kwa sasa ni mtajie jina kama wapo hawazidi wawili! Nilishituka nikajiuliza kwa nini? Nikapata shida sasa huenda Bongo muvi imekufa! Nikaanza kufanya uchunguzi nikakuta kila producer ana shoot tamthilia. Haa nilishangaa mastar waliotoka kwenye tamthilia wakiita ni maigizo wakaenda kushoot filamu ambazo pia hazikuwa na tofauti na maigizo wakirudi kufanya maigizo. Duuuh! Nikaanza kujiuliza maswali bila majibu.
Hivi wadau ni wapi tumekosea? Ni msanii, mzalishaji, msambazaji au mnunuzi wa mwisho kachoka? Taratibu kumbukumbu zangu zikanirudisha miaka minne iliyopita kabla Steven Kanumba hajafa ambapo struggle za wasambazaji kumiliki wasanii ma star zilivyo pamba moto na mastar kutoa vikwazo kwa waandaaji wadogo. Maana ulikuwa ukienda kutaka kufanya kazi utajibiwa na mkataba steps mwingine na mkataba pilipili basi tu ilikuwa vituko na wasio na mikataba pia walisema na wao wanamikataba mhuuu!
Nikakumbuka kipindi kizuri cha ushindani. Kipindia ambapo tulikuwa na wasambazaji wa kutosha. Tulikuwa na Steps na Kapico pia kulikuwa na Pili pili, Vishal na Famous Video, Ajay, Bajomba, Game 1st Quality, Churu Peace, Mwananchi, Al- Liyamy, SAS"O" Splash, Gibs Video, Tolly wood, Papazi, Proin, Whatever, GMC Wasanii,Beck Net, Criss Creation n.k hizi zote zilikuwa na ushindani na kila kampuni ilitoa muvi moja kwa wiki. Kampuni hizi zilikuwa ni kubwa na zilileta changamoto na kulifanya game liwe hot. Na kama inavyojulikana kwenye ushindani yule mwenye mtaji mkubwa aliwashinda wenzake. Akatumia mbinu zake kuteketeza wenzake leo hii ule ushindani haupo si hakuna wengine, utashindana na nani bidhaa inatoka sehemu moja. Mtu anataka awe peke yake! Radha ikapungua kwa watazamaji watu wakawa wanafanya kazi kuwahi foleni si hakuna kwingine pa kuuza.
Sasa mawazo yangu yakanirudisha ni nani kaua soko? Unapeleka muvi leo inatoka baada ya miaka miwili! Kumbe ungepeleka kwenye kampuni nyingine na ungeuza mapema! Duuh zile siku za ushindani zilikuwa nzuri ndio maana maneno midomoni yakawa mengi watu wakiisifia na kila mtu akahamasika kuwa msanii kwa nafasi yake.
Ukitazama kabla ya Kifo cha Steven Kanumba kulikuwa na kampuni nyingi sana za usambazaji tena zenye uwezo mkubwa ila baada ya kifo chake kampuni moja moja ikaanza kupoteza uwezo wa kusambaza na kuishia kufunga kampuni. Wakabaki wasambazaji wachache ambao walijikongoja na mpaka sasa msambazaji akitoa muvi tatu unatakiwa kumheshimu wengi huishia mbili tu chali. Mungu atunusuru! Swali ukitengeneza muvi unauza wapi? Mbona wasanii mastar wanakimbia kufanya muvi? Kuna tatizo gani? Au ndio upepo wa kukurupuka umeenda kwenye tamthilia? Au ni kwa sababu TV stations zimeongezeka? Midomoni mwa maproducer wengi ni ku produce tamthilia kitu ambacho kinahitaji bajeti kubwa kuliko muvi!
MUNGU BARIKI TASNIA YETU.